DKT SAMIA AIGUSA SUMBAWANGA SEKONDARI

 

DKT SAMIA AIGUSA SUMBAWANGA SEKONDARI

DKT SAMIA AIGUSA SUMBAWANGA SEKONDARI

RUKWA
Manispaa ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri zilizopokea fedha ya Ruzuku kutoka Serikali kuu kiasi cha Tsh. 1,662,200,000 kwa ajili ya miundombinu mbalimbali katika Shule za Sekondari.
Kutoka kwenye  fedha hizo  Shule ya Sekondari Sumbawanga ilipokea Tsh. 45,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu(3) vya madarasa na Tsh. 14,600,000 kwa ajili ya ujenzi wa matundu nane (8) ya vyoo
Kukamilika kwa mradi huu kumepunguza msongamano wa Wanafunzi katika vyumba vya madarasa yaliyokuwepo awali na kuepusha magonjwa ya mlipuko yatokanayo na changamoto ya vyoo.