TSH BIL 70.8 KUJENGA BARABARA MLIMBA DC
MOROGORO
Kiasi cha shilingi bilioni 70.8 kimetolewa na serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Mbingu-Chita Km 37.5 kwa kiwango cha lami iliyopo Halmashauri ya wilaya Mlimba Mkoani Morogoro .
Ujenzi wa barabara hiyo umeanza Juni 25, 2024 na unatarajiwa kutekelezwa ndani ya miezi 20 kuanzia siku ulipokabidhiwa.
