TANZANIA, URUSI KUSHIRIKIANA HUDUMA ZA ANGA
URUSI
Tanzania na Urusi zimesaini mkataba wa Ushirikiano kwenye huduma za anga utakaowezesha mataifa hayo kushirikiana katika usalama wa anga na ndege kwa viwango vya kimataifa.
Naibu Waziri wa Uchukuzi wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Poteshkin na Balozi mdogo wa Tanzania - Urusi, Balozi Fredrik Kibuta wamesaini mkataba huo huku Urusi ikitarajiwa kuanza safari za moja kwa moja za ndege kutoka Moscow hadi Dar es Salaam.
Shirika la Habari la Urusi, Sputnik limesema mkataba huo unaweka kanuni na masharti juu ya ukusanyaji kodi katika uwanja wa ndege, ushuru wa forodha na udhibiti wa ushuru.
