TSH BIL 41.39 KUTAFITI MBEGU

 

TSH BIL 41.39 KUTAFITI MBEGU

TSH BIL 41.39 KUTAFITI MBEGU

DODOMA
Serikali kupitia wizara  ya Kilimo imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 41.39 katika utekelezaji wa mikakati ya kuinua ufanisi wa sekta ya utafiti na uzalishaji wa mbegu.
Utafiti wa mbegu ni miongoni mwa maeneo sita muhimu ambayo yamepewa kipaumbele na wizara ili kuhakikisha dira iliyowekwa ya kuruhusu sekta ya kilimo kuchangia angalau 20% kwenye pato la taifa inafikiwa pia ni muhimu kwa ukuaji mzuri wa sekta ya uchumi, kwa kuzingatia kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa ukuaji wa uchumi wa nchi.
Kiasi hicho cha shilingi bilioni 41.39 kitatolewa ili kuwezesha miradi mikubwa ya ujenzi wa Benki ya kisasa katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) cha Selian mkoani Arusha.
Aidha, matumizi mengine kwenye fedha hiyo  itahusisha ufungaji wa maabara kubwa ya sayansi ya viumbe katika Kituo cha TARI Mikocheni jijini Dar es Salaam, kudhamini jumla ya wataalam wa kilimo 485 kupata elimu ya juu ya utafiti wa mbegu pamoja na kukarabati TARI yenye makao yake makuu Arusha Tengeru Center na kuifanya kuwa kituo bora cha utafiti wa bustani.
Mipango hiyo pia itahusisha kuzalisha na kusambaza kwa wakulima jumla ya miche milioni 5.7 ya muhogo katika mikoa yote ambayo zao hilo linastawi na kuendelea na kazi ya jumla ya kuweka miundombinu ya umwagiliaji katika jumla ya mashamba 19 ya utafiti, yanayochukua jumla ya hekta 1,120.