TANZAM YAWEKWA ALAMA KUONDOA HATARI
MBEYA
Serikali kupitia wizara ya ujenzi imefanya marekebisho katika maeneo hatarishi (blackspot areas) yaliyopo barabara ya TANZAM kwa kuweka alama zote muhimu za barabarani, michoro ya barabarani, kufunga taa za usalama barabarani (street lights), kupanua makutano ya barabara pamoja na kujenga njia na vivuko vya waenda kwa miguu.
Maeneo hatarishi yaliyofanyiwa marekebisho ni pamoja na Inyala Mkoani Mbeya, Kingolwira, Milima ya Iyovi, Mbuga ya wanyama ya Mikumi na Kijiji cha Mikumi Mkoani Morogoro, Picha ya Ndege, Kwa Mathias, Kongowe, Vigwaza na Chalinze Mkoani Pwani pamoja na mlima Kitonga Mkoani Iringa.
Aidha, ujenzi wa madaraja mapya ya Wami na Kibamba ambapo ajali nyingi zilikuwa zikitokea umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali za barabarani