KILA MWANANCHI ANA MITA ZA UJAZO 2,105 ZA MAJI KWA MWAKA

 

KILA MWANANCHI ANA MITA ZA UJAZO 2,105 ZA MAJI KWA MWAKA

KILA MWANANCHI ANA MITA ZA UJAZO 2,105 ZA MAJI KWA MWAKA

TANZANIA
Nchi yetu inakadiriwa kuwa na rasilimali za maji zinazofaa kwa matumizi mbalimbali za wastani wa mita za ujazo bilioni 126 kwa mwaka. 
Kiasi hicho kinahusisha maji juu ya ardhi mita za ujazo bilioni 105 na maji chini ya ardhi mita za ujazo bilioni 21 kwa mwaka. 
Kwa idadi ya watu milioni 59.8 wa Tanzania Bara kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, inaonesha kuwa kiasi cha maji kilichopo kwa kila mtu kwa mwaka ni takribani wastani wa mita za ujazo 2,105. 
Kiasi hicho kipo juu ya kiwango cha chini cha mita za ujazo 1,700 cha mahitaji ya maji kwa mtu kwa mwaka kinachokubalika kimataifa.
Hali hiyo, inaonesha kuwa nchi yetu ipo juu ya kiwango cha uhaba wa maji (water stress).