TANZANIA KUWA MWENYEJI WA WAKUU WA ANGA BARANI AFRIKA
ARUSHA
Wakuu wa usafiri wa anga kutoka kote barani Afrika wanakutana mjini Arusha, Tanzania tarehe 6 juni 2024 ili kujadili mikakati bunifu ya kukuza sekta ya usafiri wa anga barani humo.
Kufuatia Tanzania kuandaa hafla hiyo, Rais wa Kamisheni ya Usafiri wa Anga ya Afrika, Mhe. Silas Udahemuka, ametoa shukrani zake kwa Tanzania kwa kuandaa hafla hiyo huku akiwataka wajumbe kuchangamkia fursa hiyo kutatua na kuondokana na changamoto za sekta hiyo kwa njia ya mazungumzo yenye kujenga.
Mkutano huo wa utakaofanyika katika Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha, utahusisha pia kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa pia ni sehemu ya juhudi za kukuza utalii nchini Tanzania, na kuongeza mwelekeo wa kitamaduni na mazingira katika hafla hiyo.
Taarifa kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAAimesisitiza kuwa mkutano huo sio tu wa kutatua changamoto. Pia inahusu kuunda sauti ya umoja wa Kiafrika katika vikao vya kimataifa, kuhakikisha maslahi ya usafiri wa anga ya bara hili yanawakilishwa vyema na kulindwa.