TANZANIA KINARA KUUZA NYAMA QATAR

 

TANZANIA KINARA KUUZA NYAMA QATAR

TANZANIA KINARA KUUZA NYAMA QATAR

DODOMA
Taarifa kutoka Maendeleo ya Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi inasema  Qatar ndiyo nchi inayoongoza kwa kuingiza nyama ya ng’ombe kutoka Tanzania kwa kuagiza takribani 25% ya wastani wa mauzo ya nje kwa mwaka.
Hadi mwezi Mei 2024 Qatar iliagiza nyama zaidi ya 5,111.92 kutoka Tanzania  yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 13.6  (sawa na shilingi bilioni 34.680)  ambapo  idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi mwishoni mwa mwaka huu wa fedha.
Aidha kwa miaka miwili mfululizo ya 2022/23 – 2023/24 jumla ya tani 8,425.49 zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 34.69 (zaidi ya shilingi bilioni 88.459) zilisafirishwa kwenda Qatar.
Vilevile katika mwaka wa fedha wa 2023/24, Oman iliifuatia Qatar kwa kuagiza tani 3,381.52 kutoka 3,218.51 mwaka uliopita na Umoja wa Falme za Kiarabu ulikuwa na tani 2,377.10, chini kutoka 2,842.32 za mwaka 2023.
KUMBUKA:- Tanzania inasafirisha nyama ya ng’ombe kwa nchi 12 ambazo ni Bahrain, Comoro, Hong Kong—China, Jordan, Kenya, Kuwait, Oman, Qatar, Rwanda, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu (UAE) na Vietnam.