TANZANIA KUNUFAIKA NA TSH TRIL 6.6 ZA KOREA

 

TANZANIA KUNUFAIKA NA TSH TRIL 6.6  ZA KOREA

KOREA KUSINI

Juni 02, 2024 Tanzania na Jamhuri ya Korea zimetiliana saini makubaliano ya mfumo utakaowezesha Tanzania kupata mikopo ya masharti nafuu kutoka Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF) yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.5 (takribani shilingi trilioni 6.6) katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2024-2028)

Hafla hiyo ya utiaji saini imeshuhudiwa na Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake  Rais wa Korea Mhe Yoon Suk Yeol jijini Seoul nchini Korea.

Zaidi ya hayo, mataifa hayo mawili yametia saini Azimio la Pamoja la kuanzisha Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) na Mikataba miwili ya Maelewano (MoUs), ikijumuisha ugavi thabiti wa madini ya kimkakati kutoka Tanzania hadi Korea Kusini ambapo EPA inalenga kuimarisha uhusiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Korea, hasa katika maeneo kama vile biashara, uwekezaji, viwanda na usafirishaji. 

Makubaliano hayo yaliyotiwa saini ni pamoja na Ushirikiano wa Uchumi wa Bluu, ambapo Tanzania na Korea Kusini zitashirikiana katika uvuvi, usindikaji wa dagaa, ujenzi wa bandari ya uvuvi, teknolojia ya baharini na utafiti.

Ili kuongeza thamani ya madini ya kimkakati kama vile nikeli, lithiamu na grafiti, Wizara ya Madini ya Tanzania na Wizara ya Biashara, Viwanda na Nishati ya Korea Kusini zitashirikiana katika utafiti, uwekezaji, uchimbaji na kujenga uwezo

Aidha Pande hizo mbili zimetiliana saini Mkataba wa kupata mnyororo muhimu wa ugavi wa madini, pamoja na mwingine kuhusu ushirikiano wa uchumi wa bluu, kuimarisha uhusiano katika sekta ya rasilimali za baharini na uvuvi.