MIZANI 12 ZA KUDUMU ZAJENGWA
MWANZA
Serikali kupitia TANROADS, imejenga mizani 12 ya kudumu ambayo ni mizani ya Usagara West (Mwanza), Rubana (Mara - 2), Matundasi (Mbeya), Mingoyo North (Lindi), Mikumi South (Morogoro), Kamsisi (Katavi), Mdori West (Manyara Igagala (Njombe), Nyantare (Mara) na Mkolye (Tabora - 2).
Aidha mizani saba (7) inayopima magari yakiwa kwenye mwendo (Weigh in Motion) imejengwa Mikumi (2) mkoani Morogoro, Kemokouwa (Arusha -2), Mikese North (Morogoro) na Rubana (Mara – 2).
Kupitia mizani hiyo, uzidishaji wa uzito unaoruhusiwa kisheria umeshuka kutoka 0.48% kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi 0.26% kwa mwaka wa fedha 2023/24
Jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha miundombinu ya barabara zinaenda sambamba na uimarishaji wa miundombinu ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuzuia uharibifu wa miundombinu ya barabara ambayo hujengwa kwa gharama kubwa.
