KIWANJA CHA NDEGE CHA SHINYANGA KUKAMILIKA JUNI 2025
SHINYANGA
Ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Shinyanga umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwezi juni 2025 na shilingi bilioni 48.5 zinatumika katika ujenzi huo.
Kwa sasa njia za kuruka na kutua ndege, maegesho na barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani hapo zimekamilika wakati jengo la abiria uko katika hatua nzuri za ujenzi
kiwanja hicho kina urefu wa meta 2200 na upana wa meta 30 hivyo kitawezesha ndege aina ya Bombadier Q400 kutumia kiwanja hicho huku wananchi zaidi ya 240 wakipata ajira na kukamilika kwake kutachochea ukuaji wa shughuli za kilimo, madini na biashara.
Kukamilika kwa ujenzi wa kiwanja hicho kutaondoa adha kwa watumiaji wa huduma za ndege na kuchochea ukuaji wa Manispaa ya Shinyanga