TANZANIA KUFIKIA LENGO NAMBA 2 SDG 2030 (CHAKULA)

 

TANZANIA KUFIKIA LENGO NAMBA 2  SDG 2030 (CHAKULA)

TANZANIA KUFIKIA LENGO NAMBA 2  SDG 2030 (CHAKULA)

MOROGORO
Tanzania kwa sasa ina chakula cha kutosha kukidhi mahitaji ya nyumbani, na ziada inapatikana, ikionesha maendeleo makubwa ya kufikia Lengo la Maendeleo Endelevu (SDG) namba mbili ifikapo 2030, Wizara ya Kilimo imesema kupitia mkutano wa wadau wa usalama wa chakula uliofanyika Mkoani Morogoro.
Malengo ya SDG namba II inalenga kuondoa njaa, kufikia usalama wa chakula na lishe bora, na kukuza kilimo endelevu.
Taarifa ya wizara ya kilimo inasema
"Tumetekeleza hatua za kuhakikisha mipaka yetu iko wazi kwa ajili ya kuuza chakula cha ziada nje ya nchi, kulingana na lengo letu la kumaliza njaa ifikapo 2030," imesema taarifa hiyo.