JAPAN YAIPA HEKO TANZANIA KWA UWEKEZAJI
DAR ES SALAAM
Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Kiyoto Tsuiji ameitaja na kuipongeza Tanzania kuwa nchi yenye matumaini kwa ukuaji wa uwekezaji akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pande hizo mbili kati ya nchi hizo mbili, hii ni kupitia mkutano na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ubalozi wa Japan.
Pongezi za Japani zinakuja wakati ambao ina miongo minne katika uwekezaji wake nchini Tanzania wenye thamani ya dola za Marekani milioni 42.70 (kama shilingi bilioni 111) huku ukigusa sekta muhimu za kiuchumi zikiwemo viwanda, ujenzi wa biashara na kilimo.
Aidha, balozi huyo ameipongeza Serikali chini ya Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji yanayoainishwa na Diplomasia ya Uchumi ambayo inaongeza fursa kwa nchi zote mbili.
ZINGATIA:-Mageuzi ya Sheria Mpya ya Uwekezaji ya 2022 yanavutia wawekezaji kote ulimwenguni ikiwa ni pamoja na Wajapani na hivyo kuimarisha uhusiano wa kiuchumi.