TANZANIA, GUINEA -BISSAU KUKUZA KILIMO CHA KOROSHO
DAR ES SALAAM
Tanzania na Guinea Bissau zimekubaliana kukuza kilimo cha korosho, biashara na uwekezaji,uchumi wa buluu, ushirikiano katika sekta za afya na elimu, ulinzi na usalama pamoja na masuala ya kimataifa.
Uthibitisho wa makubaliano hayo umetolewa na Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais Wa Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló wakati wakizungumza na vyombo vya habari juni 22, 2024 Ikulu Jijini Dar e s salaam.
Mhe Rais Samia amesema” nchi zetu mbili Guinea Bissau na Tanzania ni wazalishaji wakubwa wa korosho , hilo ndilo eneo ambalo tumesema tuanze ushirikiano hasa kwenye kufanya utafiti na kuongeza thamani ya mazao yetu”
Aidha Mhe Rais Samia amesema Bara la Afrika lipo mbioni kuhakikisha linafungua eneo huru la biashara lengo likiwa ni kukuza zaidi kiwango cha biashara kati ya nchi za Afrika na kuanzishwa kwa soko hilo kutachochea ukuaji wa viwanda,uongezaji wa thamani wa mazao pamoja na kuleta ajira kwa vijana