DKT SAMIA AMPONGEZA RAIS MTEULE WA MEXICO, MHE CLAUDIA
KOREA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amempongeza Rais mteule wa Mexico Mhe Claudia Sheinbaum(kupitia chama cha Movement for National Regeneration -Morena) kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Nchi hiyo kufuatia uchaguzi uliofanyika Juni 2, 2024 na kutangazwa na Taasisi ya Taifa ya uchaguzi ya Mexico (INE) kuwa mshindi kwa kupata 58% kati ya 60% ya kura zilizopigwa.
Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii Mhe Rais Samia ameandika “On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to Her Excellency Claudia Sheinbaum, President-elect of Mexico, on your historic victory in the 2024 Mexican general election. Madam President-elect, you have my best wishes (Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Claudia Sheinbaum, Rais Mteule wa Mexico, kwa ushindi wako wa kihistoria katika uchaguzi mkuu wa 2024 nchini Mexico. Mheshimiwa Rais Mteule, nakutakia kila la kheri).
BimkubwaTanzania tunaungana na Mhe Rais Dkt Samia kukutakia kila la kheri katika majukumu yako mapya ya kuwatumikia wananchi wa Mexico.
