MIRADI YA TSH BIL 82 INATEKELEZWA TEMESA
DODOMA
Kwa kipindi cha uongozi wa Dkt. Samia Suluhu madarakani TEMESA imeanzisha na imeendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya vivuko yenye Thamani ya shilingi bilioni 82.
kati ya shilingi bilioni 82 , 90% ya kazi zinafanywa na wakandaradi wazawa ambapo shilingi bilioni 42 zimeelekezwa kujenga vivuko vipya ambavyo vitaenda kutoa huduma kwenye maeneo ambayo wananchi walikuwa wanatumia mitumbwi kuvuka na maeneo mengine ambayo yalikuwa yamekosa kabisa huduma za vivuko baadhi yakiwa maeneo ya Ijinga - Kihangala, Bwiro-Bukondo, Buyagu - Mbalika ambapo ndani ya miaka mitatu vivuko vimeendelea kujengwa na ujenzi umefikia 80%.