DKT SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA KOREA NA AFRIKA
KOREA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo juni 4 amewasili Kintex, nje kidogo ya Jiji la Seoul, nchini Korea kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Korea na Afrika.
Mkutano huo wa siku mbili (tarehe 4 na 5) umezikutanisha nchi 48 za Afrika ambapo mataifa 25 kati yao yatawakilishwa na wakuu wao wa nchi ( Waheshimiwa Marais) huku Rais Yoon Suk Yeol akiwa mwenyeji wa mikutano hiyo, hii ni kwa mujibu wa Naibu Mshauri Mkuu wa Usalama wa Kitaifa wa Jamhuri ya Korea bwana Kim Tae-hyo
“Mkutano huu utakuwa mkutano mkubwa zaidi wa kilele wa pande nyingi tangu kuzinduliwa kwa serikali ya Yoon Suk Yeol na mkutano wa kwanza wa mataifa mbalimbali Korea Kusini utakuwa mwenyeji unaohusisha Afrika,” Kim amesema.
Nae Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea, Bw Chung Byung-won, amesema “Mkutano huo utaanzisha ushirikiano wa kunufaishana, wa kimkakati na wa kudumu kwa muda mrefu na Afrika. Tunatafuta kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na ukuaji na tukio hili litatoa fursa nzuri kwa nchi za Afrika kufaidika na teknolojia ya kibunifu ambayo Korea inayo kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo” amesema bwana Chung.
Aidha Mikutano hiyo itafanyika wakati wa chakula cha mchana au chakula cha jioni kwa viongozi wa Tanzania, Sierra Leone, Ethiopia, na Mauritania.
