VIBALI 11,258 VYA KUUZA MADINI VYATOLEWA

 

VIBALI 11,258 VYA KUUZA MADINI VYATOLEWA

VIBALI 11,258 VYA KUUZA MADINI VYATOLEWA

TANZANIA
Katika Mwaka 2023, jumla ya vibali 11,258 vya kuuza madini nje ya nchi vilitolewa ikilinganishwa na vibali 10,318 vilivyotolewa Mwaka 2022. 
Ongezeko la vibali hivyo kwa kiasi kikubwa limetokana na kuongezeka kwa uhitaji wa madini ya vito na makaa ya mawe nje ya nchi. 
Aidha, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, jumla ya vibali 115 vya uingizaji madini nchini vilitolewa ikiwa ni hatua mojawapo ya kusimamia na kudhibiti biashara ya madini nchini.