UWEKEZAJI WA DKT SAMIA WAWAVUTA WA- SIERRA LEONE NCHINI
DAR ES SALAAM
Mganga Mkuu wa Serikali ya Sierra Leonne Dk. Sartie Mohamed Kenneh akiambatana na Wataalamu wa Afya kutoka nchi hiyo wamewasili nchiniTanzania (Bohari ya Dawa –MSD na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete -JKCI) kwa lengo kujifunza ubunifu ambao MSD wamekuwa nao katika kufanya shughuli zao za kuzalisha, kununua, kutunza,kusambaza dawa,uhimilivu na matumizi ya Tehama pia na uwekezaji wa vifaa tiba uliofanyika na Mhe Rais Dkt Samia.
Malengo mengine ni kubadilishana uzoefu kuhusu shughuli za ugavi, uhifadhi, uendeshaji, ununuzi, huduma kwa wateja, sera, udhibiti ubora, pamoja na mambo mengine yanayohusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.
Akizungumza Mganga Mkuu wa Serikali ya Sierra Leonne Dk. Sartie Mohamed Kenneh amesema wamekuja kujifunza na kuangalia mifumo ya afya hali itakayoasaidia uboreshaji wa huduma katika nchi yao.
“Tunachangamoto ndio maana tuko hapa na tumeona Tanzania ni sehemu ya kujifunza hata kama sio kwa asilimia 100 lakini kuna vingi tumeona na tumelinganisha na sisi na tumeona tumejifunza” amesema Dk Kenneh
Aidha ujio wa wageni hao nchini ni ishara kwamba kama nchi imeboresha na kuimarisha huduma za afya na vifaa tiba kupitia mpango wa utalii tiba wenye lengo la kukaribisha wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kutibiwa Tanzania.
