UUNGANISHAJI MAGARI KODI YASHUKA KUTOKA 30% HADI 10%
DAR ES SALAAM
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imepunguza kodi kwa sekta ya uunganishaji wa magari kutoka 30% hadi 10 kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2024-2028
Taarifa hiyo imetolewa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan leo tarehe 9 Mei 2024 wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kiwanda cha Saturn Corporation Limited kilichopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam
Dkt Samia amesema lengo la serikali kutoa punguzo hilo ni kuchochea uwekezaji kwenye sekta hiyo na kuongeza ajira kupitia viwanda na kurahisisha upatikanaji wa magari yatakayosaidia kwenye shughuli za kiuchumi hususan kilimo, na biashara.
Aidha Dkt Samia amesema ufunguzi wa kiwanda hicho ni alama tosha kwamba sera za uwekezaji zinaleta matokeo.
