TAZARA YAVUNA TSH BIL 8.91 USAFIRISHAJI MIZIGO
TANZANIA
Ushirikishaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa shirika la reli (TAZARA) umeisadia Tanzania kuvuna kiasi cha shilingi bilioni 8.91 kutokana na kampuni ya Ms Calabash Freight Limited na Ms African Inland Container Depot (AFICD) kulipia tozo.
Hadi kufikia Machi 2024, TAZARA ilisafirisha jumla ya tani za mizigo 251,264 ikilinganishwa na tani 235,071 zilizosafirishwa katika kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha 2022/23 sawa na ongezeko la asilimia 6.89.
Aidha treni za abiria zinazofanya safari kati ya Dar es Salaam na New Kapiri Mposhi na ile inayosafiri kati ya stesheni za Kidatu na Makambako zilisafirisha jumla ya abiria 672,006.
Pia Treni ya Jijini Dar es Salaam inayofanya safari zake kati ya Stesheni ya TAZARA hadi Stesheni ya Mwakanga - Pugu jijini Dar es Salaam ilisafirisha abiria 1,582,833 ikilinganishwa na abiria 1,447,738 waliosafirishwa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2022/23 sawa na ongezeko la 9.33%
[07:31, 5/20/2024] Asina Nanyanga: Habari ya asubuhi Team,
nawapa taarifa kwamba kutokana na changamoto za Internet ofisini kwetu, naomba tusiingie leo Mei 20 wakati uongozi unashirikiana na mafundi kutafuta suluhisho la kudumu la Internet.
Wakati na muda wowote suala hili likipatiwa ufumbuzi tutarudi ofisini kuendelea na majukumu yetu.
kwa mwenye nafasi ya kufanya kazi akiwa nje ya ofisi na atatakiwa afanye, pia majukumu yataendelea kutolewa pale inapotakiwa kuwa hivyo.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
