MAGARI, PIKIPIKI KUIMARISHA USALAMA MIPAKANI
MBEYA
Serikali kupitia wizara ya Afya imeendelea kuimarisha huduma za afya katika vituo vya Afya mipakani ili viweze kutoa huduma madhubuti na kwa ufanisi kwa kusambaza magari 16 na pikipiki 20 katika vituo 36 vya afya mipakani.
Aidha serikali kupitia wizara ya afya imefanikiwa kununua Vipima joto (Walkthrough Thermoscaners) 10 ambavyo vimesambazwa katika mipaka iliyopo mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Mara, Mbeya na Songwe kwa ajili ya kuendelea kuimarisha uchunguzi kwa wasafiri.
Aidha, Wizara imeendelea kuimarisha ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza katika maeneo ya mipakani ikiwa ni pamoja na ukarabati wa jengo moja (1) kwa ajili ya kuwatenga wasafiri washukiwa wa magonjwa ya kuambukiza (Isolation unit) katika mpaka wa Mutukula mkoani Kagera pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kudumu ya kunawia mikono (Mass Hand Washing Facilities) inayojengwa katika mpaka wa Rusumo na bandari ya Kigoma ili kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza.
