TZ, ZAMBIA KUIMARISHA USAFIRI, BIASHARA

 

TZ, ZAMBIA KUIMARISHA USAFIRI, BIASHARA

TZ, ZAMBIA KUIMARISHA USAFIRI, BIASHARA

LUSAKA
Zambia na Tanzania zimeeleza dhamira yao ya kushirikiana katika kuimarisha usafirishaji wa mizigo ya makontena na biashara kati ya nchi hizo mbili jirani.
Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Zambia, Bw Frank Tayali, amefichua azma ya nchi ya Zambia  ya kuimarisha usafiri na nchi jirani, ikiwa ni pamoja na Tanzania, wiki iliyopita wakati akifunga Kongamano la tatu la Usafiri na Usafirishaji la Zambia lililofanyika Lusaka nchini Zambia.
Bw Tayali amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha ukuaji wa uchumi na nchi jirani,hivyo Zambia inakamilisha mipango ya maendeleo ya kikanda kuwa ni kiungo cha mkakati wa mtandao wa ukanda katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA), kwa kutumia hadhi yake ya kuunganishwa kwa ardhi kuwezesha biashara na kuhudumia nchi jirani.
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya wizara ya uchukuzi amesema mkutano huo umeiwezesha Tanzania kufanya uonekanaji wa miundombinu mbalimbali ya usafiri iliyopo.
Bwana Mkingule amefafanua kuwa miundombinu muhimu iliyotangazwa katika mkutano huo ni ndege na bandari za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) chini ya TPA.
Mkutano huo wa siku mbili wenye kaulimbiu ya “Kuunganisha Zambia na SADC kwa ardhi ili kuwezesha biashara, uwekezaji na urahisi wa usafirishaji wa bidhaa na watu,” ulioanza Aprili 4 mwaka huu, ulileta makundi mbalimbali ya taasisi za sekta ya usafiri, ikiwemo TPA kama mfadhili mwenza.