FILAMU NYINGINE YA DKT SAMIA KUZINDULIWA MEI,2024
TANZANIA
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi wamerekodi filamu yenye hadhi ya kimataifa ya kutangaza utalii inayoitwa Amazing Tanzania, filamu ambayo imechezwa pia na Mchezaji Filamu nguli kutoka nchini China ajulikanaye kwa jina la Jin Dong.
Filamu hiyo imeandaliwa kwa lengo la kutangaza utalii wa Tanzania Bara na Zanzibar hususan kwa soko la China na inatarajiwa kuzinduliwa Mei, 2024.
Filamu ya Amazing Tanzania inakuwa filamu ya pili kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hasssan baada ya kucheza Royal Tour na kuliingizia taifa fedha za kigeni kutoka Dola za Marekani bilioni 2.53 mwaka 2022 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.37 mwaka, 2023 sawa na ongezeko la 33.5% na kuongeza idadi ya watalii wa kimataifa kutoka 1,454,920 mwaka 2022 hadi kufikia watalii 1,808,205 mwaka 2023 sawa na ongezeko la 8.4%