TZ, DENMARK KUFUNGA MKANDA MABADILIKO YA TABIANCHI.
DODOMA
TANZANIA na Denmark zimejitolea kushirikiana katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Chanzo:- wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), wakati wa mkutano hivi karibuni Jijini Dodoma na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Sera ya Dunia ya Hali ya Hewa wa Denmark, Bw. Dan Jørgensen.
Wizara ya Muungano na Mazingira ilimueleza waziri wa Denmark kuhusu dhamira ya serikali ya Tanzania katika kuendeleza upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kama njia ya kutatua changamoto ya ukataji miti na kuhakikisha uhifadhi wa mazingira endelevu.
Kwa upande wake Waziri Jørgensen ameeleza kuwa ni wakati sasa wa kudumisha uhusiano imara kati ya nchi hizo mbili ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na changamoto za kimazingira zinazoikabili dunia.
Aidha amesisitiza kuwa mabadiliko ya tabianchi yana athari kubwa kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania na kuathiri shughuli za kiuchumi hasa kilimo hiivyo ni muhimu kuunganisha nguvu ili kukabiliana na changamoto hizo.