SERIKALI YAWAPA BEGA LA KUEGEMEA RUFIJI,KIBITI PWANI

SERIKALI YAWAPA BEGA LA KUEGEMEA RUFIJI,KIBITI

SERIKALI YAWAPA BEGA LA KUEGEMEA RUFIJI,KIBITI

PWANI
SERIKALI imewapa bega la kuegemea waathirika wa mafuriko katika wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani kwa kiwango cha juu na cha karibu kwa kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji mkubwa wa huduma muhimu ikiwemo malazi, chakula na afya.
Kufuatia mafuriko hayo Mhe Rais Dkt Samia akizungumza wakati wa sherehe ya Eid (kupitia baraza la Baraza ) jijini Dar es Salaam Jumatano, alitoa ujumbe wake wa kuwafariji wananchi walioathiriwa na mafuriko katika Mkoa huo, na kuwahakikishia kwamba serikali itapeleka msaada wa haraka ili kutatua changamoto zinazowakabili, agizo ambalo limeaanza kutekelezwa kwa kusambaza vyakula aina ya unga wa mahindi na maharage huku wito ukitolewa chakula hicho kinasambazwa kwa wananchi walioathirika
Vilevile serikali imewaagiza watumishi wa afya na wataalam wa ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii pamoja na wizara ya Maendeleo ya Jamii kuwabaini watu walio katika makundi maalum wakiwemo kina mama wajawazito, wajane, watoto na wazee wanaohitaji msaada wa haraka katika kipindi hiki.
Kufuatia uharibifu mkubwa wa miundombinu ya umeme,tayari timu ya wataalamu kutoka Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) inaendelea na tathmini ili kubaini na kushughulikia kwa haraka masuala hayo ili kuhakikisha maisha yanarejea katika hali ya kawaida.
POLENI SANA PWANI, NI SUALA LA MUDA TU
#Hilinalolitapita