MUSOMA (V) MAJISAFI NI UHAKIKA

 

MUSOMA (V) MAJISAFI NI UHAKIKA

MUSOMA (V) MAJISAFI NI UHAKIKA

MARA
Mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 4 umesainiwa Musoma vijijini  Mkoani Mara kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya maji safi
Utiaji saini huo umefanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Kwikuba, ukihusisha Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na mkandarasi, Otonde Construction and General Supplies Limited.
Mradi huo unatarajiwa kuchimba maji kutoka Ziwa Victoria na utawanufaisha wakazi wa Kata ya Busambara, vikiwemo vijiji vya Kwikuba, Maneke, na Mwiringo, pamoja na Kata ya Kiriba inayojumuisha vijiji vya Bwai Kumsoma, Bwai Kwitururu na Kiriba.
Akizungumzia mradi huo mkazi wa Kijiji cha Kwikuba Bi Mwajuma Chacha ameipongeza serikali kwa kuwapelekea mradi wa maji katika kijiji chao na kueleza kuwa utamaliza miongo mingi ya uhaba wa maji.
“Kwa muda mrefu, wanawake katika kijiji chetu wamekuwa wakihangaika usiku na mchana kutafuta maji. Mradi huu utatusaidia,” amesema Bi Mwajuma.
Serikali imeeleza mikakati na mipango ya kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote kwa kufanya uwekezaji katika miundombinu ya maji, kama vile mabomba, mitambo ya kutibu maji, na mitandao ya usambazaji, unapewa kipaumbele ili kuhakikisha upatikanaji wa maji wa uhakika kwa jamii.
Aidha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Tanzania (FYDP III) unajumuisha mkazo katika kuboresha huduma za maji nchini kote.