TZ, UHOLANZI, CHINA KUSHIRIKIANA MAZAO YA MBOGAMBOGA
ARUSHA
Serikali ya Tanzania, China na Uholanzi zitaendelea kushirikiana kukiendeleza Kituo cha Taasisi ya Utafiti na Uendelezaji wa Mazao ya Mbogamboga Duniani cha (World Vegetable Centre) ili kukidhi mahitaji ya wakulima.
Chanzo:- wizara ya kilimo, kwenye uzinduzi wa Benki ya Afrika ya vinasaba ya mbegu za mboga za asili katika kituo cha Worldveg kilichopo Tengeru mkoani Arusha
Hadi sasa benki hiyo inahifadhi aina 5,000 za mbegu huku lengo likiwa kufikia aina 15,000 ifikapo mwaka 2025/26 ya mbegu zinazopaswa kuhifadhiwa katika benki, ikiwa msingi wa kituo hicho ni kwa ajili ya wakulima duniani na sio Afrika pekee
Aidha Benki ya Vinasaba vya mbegu Afrika ni benki pekee Afrika nha pili Kidunia kwa uhifadhi wa mbegu za asili za mboga mboga kwa maslahi ya wakulima.
