TANZANIA, FINLAND KUBORESHA ICT VYUO VIKUU
DAR ES SALAAM.
Vyuo vikuu vya juu nchini Tanzania na Finland vinashiriki katika majadiliano kabla ya kufanya upya Mkataba wa Makubaliano (MoU) unaolenga kuweka njia ya utekelezaji wa mradi wa teknolojia ya Geospatial-ICT (GeoICT4e).
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Turku cha Finland tayari vimesaini mkataba mpya wa utekelezaji wa mradi huo, huku vyuo vingine vya ndani kikiwemo Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kikiwa katika maandalizi ya mwisho kabla kusaini Makubaliano yao.
Ujumbe wa watu 13 kutoka Finland uliokuja jijini Dar es Salaam, siku za hivi karibuni umeeleza matumaini yake kuwa majadiliano kati ya vyuo vikuu vya Tanzania na vya Finland yatafungua mwelekeo mpya wa manufaa kwa pande zote mbili, pia kati ya taasisi zinazohusika lakini pia kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Finland.
