SERIKALI YAIGUSA MOROGORO KWA MIRADI MIKUBWA
MOROGORO
Serikali ya awamu ya sita inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya Kitaifa Mkoani Morogoro ikiwemo Ujenzi wa Barabara ya Mikumi - Kidatu – Ifakara (sehemu ya Kidatu – Ifakara, (km 66.9) kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa Daraja la Ruaha Mkuu ambao umefikia 86% za utekelezaji
Hadi sasa Mkandarasi amekamilisha km 55.67 za lami kati ya km 66.9 zinazotakiwa kwa mujibu wa Mkataba, Pia inaendelea na Ujenzi wa barabara ya Dumila – Kilosa – Mikumi (km 142) kwa kiwango cha lami (sehemu ya Rudewa – Kilosa km 24) kwa kutumia fedha za ndani.
Aidha Mkandarasi amekamilisha ujenzi wa kilometa 22.05 na imekabidhiwa na inatumika, pia ujenzi wa madaraja matatu ya Kobe, Wailonga na Mazinyungu na kwasasa unaendelea na kazi ya km 0.75 ya maungio ya madaraja hayo.
