KARIBUNI NYUMBANI RAMADHANI BROTHERS

 

KARIBUNI NYUMBANI RAMADHANI BROTHERS

KARIBUNI NYUMBANI RAMADHANI BROTHERS

DAR ES SALAAM.
Magwiji sarakasi kutoka Tanzania, Ramadhani Brothers, wamerejea nyumbani leo, kufuatia ushindi wao wiki mbili zilizopita kwenye michuano ya Mabingwa wa Dunia ya Fantasy League ya American Got Talent (AGT).
Mapokezi ya Ramdhan Brothers yamefanyika na serikali kupitia ujumbe wa Wizara ya Sanaa, Michezo, na Utamaduni pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuwasili, ndege iliyowabeba wawili hao ilipokea salamu ya maji, ikiashiria heshima kwa mafanikio yao katika kukuza jina la nchi ulimwenguni.
KUMBUKA:- Ndugu hao wawili walinyakua taji hilo baada ya kuwashinda washindi wengine tisa wa fainali, wawili kati yao walikuwa wakichuana na timu ya Howie, huku waliosalia wakiwa kwenye timu za waamuzi Simon Cowell, Mel B, na Heidi Klum, na kupata taji hilo lililokuwa likitamaniwa.
Kwa mafanikio yao makubwa, wawili hao walipokea jumla ya dola za Kimarekani 250,000 (takribani shilingi milioni  636)