JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA RUFAA SIMIYU SASA NI 95%

 

JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA RUFAA SIMIYU  SASA NI 95%

JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA RUFAA SIMIYU  SASA NI 95%

SIMIYU
Ujenzi  wa jengo la Mama na Mtoto  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu  utekelezaji wake sasa umefikia 95%  ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuboresha huduma za afya ya Mama na Mtoto kama Kipaumbele cha Sekta ya Afya.
Jengo hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kubeba vitanda 140 vya kuhudumia wajawazito na watoto hivyo  litasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuboresha afya ya jamii kwa ujumla.
Aidha kukamilika kwa jengo hili ni hatua muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu kuhusu afya ya uzazi na mtoto, na inaonesha dhamira ya serikali katika kuboresha huduma za afya nchini
FAIDA:- Jengo hili pamoja na kupunguza gharama na muda wa kusafiri kwa wagonjwa,litaongeza upatikanaji wa huduma za afya, na kuboresha afya ya uzazi na watoto.