WANANCHI SONGEA HAWATEMBEI TENA KM 3 KUFUATA MAJI
RUVUMA
WANANCHI wa kijiji cha Lyangweni kata ya Litapaswi Halmashauri ya wilaya Songea mkoani Ruvuma,wameanza kupata huduma ya maji safi na salama kwa mara ya kwanza tangu nchi ipate Uhuru.
Hatua hiyo imekuja baada ya serikali kupitia wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) wilaya ya Songea, kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji ya bomba uliogharimu Sh.milioni 618.
Kukamilika kwa mradi huo,umeanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi 2,159 wa kijiji hicho na kumeleta nafuu kubwa kwa wananchi ambao kwa muda mrefu walitembea zaidi ya kilomita 3 kila siku kwenda kuchota maji kwenye mito na vyanzo vingine vya asili.
