DKT SAMIA AKUTANA NA MFALME HARALD V, NA MALKIA SONJA.
NORWAY
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ya kitaifa ya siku mbili Nchini Norway kuanzia (LEO) Februari 13 hadi 14, 2024 baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Mfalme Harald V na Malkia Sonja wa Norway.
Kufuatia mwaliko huo, Mhe Rais Samia amewasili Norway na kupokelewa kwenye kasri la kifalme jijini Oslo na kukutana na wenyeji wake Mfalme Harald V na malkia Sonja, pia Dkt Samia akiwa kwenye kasri hilo amekagua Gwaride la Heshima na kuweka shada la maua katika Mnara wa Kumbukumbu wa Taifa Oslo Nchini Norway.
Ziara ya Dkt Samia Norway inalenga kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Norway kupitia sekta mbalimbali zikiwemo biashara, uwekezaji, nishati kama mafuta na gesi, elimu na masuala ya kodi na utawala bora.
Kuimarisha na kukuza sekta ya nishati hususan kutekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini, kushirikiana katika program za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, kukuza sekta za biashara, uwekezaji na utalii.
ZINGATIA:-Dkt Samia atashiriki Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Norway pamoja na Kogamano la Nishati la Oslo.
#BimkubwaNorway
#Diplomasianimtaji
