UGANDA KUTUMIA BANDARI YA DAR KUSAFIRISHA MAFUTA

 

UGANDA KUTUMIA BANDARI YA DAR KUSAFIRISHA MAFUTA

UGANDA KUTUMIA BANDARI YA DAR KUSAFIRISHA MAFUTA

DAR ES SALAAM
Uganda inajadiliana na Tanzania kuagiza bidhaa zake zote za mafuta kupitia bandari ya Dar es Salaam, jambo ambalo litamaanisha kukomesha uagizaji wa bidhaa kupitia bandari ya Mombasa ya Kenya
Chanzo:-  wizara ya Nishati nchini Uganda kupitia mahojiano na Reuters siku ya Alhamisi (tarehe 15,Februari,2024)
Uganda haijaridhishwa na mfumo wa muda mrefu ambapo makampuni ya mafuta ya Uganda yananunua 90% ya bidhaa zao kupitia makampuni shirikishi nchini Kenya.
Kwa kujibu wa taarifa ya wizara ya nishati ya nchini Uganda inasema nchi hiyo ilitangaza mnamo Novemba kuwa itakabidhi haki za kipekee za usambazaji wa bidhaa zote za petroli kwa kitengo cha mfanyabiashara wa nishati duniani Vitol.
Uganda kwa sasa inaagiza 90% ya bidhaa zake za petroli iliyosafishwa kupitia bandari ya Mombasa ambapo kupitia majadiliano yanayofanyika wanapanga kutumia bandari ya Dar es Salaam ili kujipunguzia gharama za uagizaji wa bidhaa za mafuta kutokana na kukatwa kiasi  kikubwa cha kodi kwenye bandari ya Mombasa, pamoja na sababu za kikodi, pia hatua hiyo imechagizwa na ufanisi ulioongezeka kwenye bandari ya Dar es Salaam.