TANZANIA YAIFUNDISHA BURUNDI KUHUSU PPRA

 

TANZANIA YAIFUNDISHA BURUNDI KUHUSU PPRA

TANZANIA YAIFUNDISHA BURUNDI KUHUSU PPRA

IRINGA
Serikali ya Tanzania kupitia mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeisaidia nchi ya Burundi kuchota maarifa ya matumizi ya mfumo mpya wa manunuzi wa kielekroniki wa Tanzania (NeST) katika maandalizi yake ya kuachana na taratibu za manunuzi za jadi zinazotumia karatasi, Hii ni kupitia mafunzo ya wiki moja yaliyofanyika na PPRA Tanzania katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, mjini Iringa.
Mfumo huo wa NeST kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Tanzania, Eliakim Maswi una uwezo mkubwa wa kudhibiti rushwa, mchakato wa zabuni kuchelewa na kuongeza uwazi na ufanisi wa zabuni katika manunuzi ya sekta ya umma.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa PPRABurundi, Jean-Claude Nduwimana amesema “Tunawashukuru sana watanzania kwa kutupokea na kutupa fursa ya kujifunza kuhusu mfumo wa manunuzi wa kielektroniki, Mafunzo haya ni sehemu ya maandalizi yetu ya kutoka kwenye mfumo wa zamani na kuingia katika matumizi ya mfumo wa kidigitali,” amasema  Jean-Claude Nduwimana.
Aidha Nduwimana ameongeza kwamba mafunzo hayo ni muhimu sana kwao kwa kuzingatia kwamba tayari nchi yao imeanza kuunda mfumo mpya wa manunuzi utakaotumia mfumo wa kielektroniki kaama ilivyo Tanzania.
“Tunatarajia mfumo huu utaongeza uwazi katika ununuzi wa umma, usimamizi mzuri wa fedha za umma, kudhibiti vitendo vya rushwa, ufuatiliaji kukidhi sheria, uwajibikaji na udhibiti wa manunuzi”