DAR,LUSAKA KUIMARISHA USALAMA

 

DAR,LUSAKA KUIMARISHA USALAMA

DAR,LUSAKA KUIMARISHA USALAMA

DAR ES SALAAM
Dar, Lusaka wakubali kuimarisha usalama, kupambana na biashara ya dawa za kulevya
Tanzania na Zambia zimetiliana saini makubaliano ya kuongeza vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na uhamiaji haramu pamoja na kuimarisha ulinzi mipakani.
Makubaliano hayo yametiwa saini katika kikao cha pili cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania/Zambia (JPCDS) Dar es salaam Februari 14,2024
Chanzo:- Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi ya Zambia Bw Norman Chipakupaku na Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (wizara kutoka Tanzania)
Kikao hicho kilihitimishwa kwa makubaliano na maazimio hayo ambayo ni pamoja na kuhakikisha yanatekelezwa yale yote yaliyokubaliwa katika kikao cha kwanza kilichofanyika mwaka jana na kikao cha pili, kwa maendeleo ya nchi zote mbili.