TSH BIL 96 KUJENGA BARABARA KM 50,LITUHI-NDUMBI
RUVUMA
Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 96 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Lituhi kuelekea Bandari ya Ndumbi yenye urefu wa kilometa 50 kwa kiwango cha lami.
Ujenzi wa barabara hiyo utawezesha meli za mizigo hasa makaa ya mawe ziweze kupakia kupitia Bandari ya Ndumbi kwenda sehemu mbalimbali za nchi yetu na nchi jirani za Malawi na Msumbiji.