TSH BIL 6.4 KULETA MAJI WILAYA TATU SHINYANGA

 

TSH BIL 6.4 KULETA MAJI WILAYA TATU SHINYANGA

TSH BIL 6.4 KULETA MAJI WILAYA TATU SHINYANGA

SHINYANGA
Serikali kupitia wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Shinyanga imewasainisha wakandarasi mikataba saba ya miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6.4 itakayotekelezwa katika wilaya tatu za Shinyanga, Kishapu na Kahama.
Mikataba  sita ni miradi ya maji ambayo itatekelezwa kwa kipindi tofauti huku mkataba mmoja ukiwa wa ununuzi wa mabomba na viungio.
Mwaka uliopita walitumia Sh bilioni 28.9 katika utekelezaji wa miradi ya maji 33 pia kuna vyombo vya watumia maji (CBWSO) 29 ambavyo vimefundishwa utumiaji wa mifumo ya Kielektroniki katika ukusanyaji wa fedha.
Mkoa wa Shinyanga una vijiji 506 ikiwa vijiji 58 tu ndiyo havina maji ambapo wananchi wake wanatumia maji kutoka vijiji jirani vyenye mabomba huku Serikali ikiendelea kutatua changamoto hiyo.