WATALII 70,186 WALITEMBELEA ZANZIBAR MWAKA 2023
ZANZIBAR
Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali (OCGS)-Zanzibar imetoa orodha ya watalii wa kimataifa waliofika Kisiwani humo, ambayo inaonesha kuwa Desemba 2023 idadi hiyo iliongezeka na kufikia 70,186 ikilinganishwa na wageni 57,296 Novemba, 2023.
Taaarifa kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali zinasema kila mwezi watalii 638,498 wa kimataifa waliingia Zanzibar katika kipindi chote cha mwaka jana (Januari hadi Desemba), kutoka kwa wageni 548,503 mwaka 2022.
Katika watalii hao, Italia inaongoza kwa kupeleka watalii zaidi kwa 12.3% ya waliofika, ikifuatiwa na Ufaransa na Poland, India, Urusi, Israel, China, na Ukraine.
Shukrani kwa filamu ya Royal Tour ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, na kuboresha mazingira kwa watalii ikiwa ni pamoja na barabara bora kwa maeneo ya vivutio vya watalii.