MVOMERO WAPOKEA DAWA NA VIFAA TIBA VYA TSH BIL 1.61
MOROGORO
Serikali ya awamu ya sita imepeleka dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.61 kwa ajili ya vituo vya afya na hospitali za wilaya ya Mvomero Katika Mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya Vifaa tiba hivyo na dawa zitasambazwa katika vituo vya afya vipya kikiwemo kituo cha Mlali, Dakawa na Mziha.