CHATO YATENGEWA TSH BIL 1.8 MTANDAO WA MAWASILIANO

CHATO YATENGEWA TSH BIL 1.8 MTANDAO WA MAWASILIANO 

GEITA

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imetenga takribani shilingi bilioni 1.8 ili kuunganisha Wilaya ya Chato na mtandao wa kitaifa wa mawasiliano.CHANZO:- Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Lengo kuu la mradi huo ni kuimarisha mfumo wa mawasiliano,ulinzi na usalama wa Chato, kuruhusu wakazi na taasisi nyingi zaidi kupata huduma kwa urahisi.

KUMBUKA :- Serikali inajenga jumla ya minara 758 nchi nzima ili kuimarisha huduma za mawasiliano na itakamilika ifikapo Mei 2025 kabla yakuanza kwa ujenzi wa awamu ya pili, utakaojumuisha minara ya ziada 636, ikiwemo minara 21 maalumu kwa ajili ya huduma za utangazaji.