DAR YAPEWA TSH BIL 52 KUIMARISHA SEKTA YA AFYA
DAR ES SALAAM
Serikali imeupatia mkoa wa Dar es salaam kiasi cha shilingi bilioni 52 kwa ajili ya kuimarisha sekta ya afya na hadi sasa fedha hizo zinajenga vituo vipya vya afya, uboreshoji wa miundombinu, vifaa tiba, utoaji huduma huku utekelezaji wa miradi mingine mipya ukiendelea.
Uwekezaji huo unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta ya afya umeleta mapinduzi makubwa ya utoaji huduma kwa wananchi.