MADAKTARI WA BMH NA UHOLANZI KUWAGUSA WAZEE NCHINI
DODOMA
Serikali kupitia hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) yenye makao yake makuu Dodoma, imeungana na madaktari bingwa kutoka Uholanzi kufanya kambi maalum ya siku kumi na tatu ya kutoa huduma ya upasuaji wa moyo kwa wazee nchini.
kambi hiyo itaanza tarehe 12 hadi 29 Februari 2024 kwa lengo la kutoa huduma kwa wale wanaohitaji upasuaji wa moyo. Na huduma hiyo itatolewa kuanzia saa mbili asubuhi katika kliniki ya moyo.
BMH imeanzisha wataalamu kadhaa na huduma za kitaalam ambazo zimesaidia nchi kuokoa mabilioni ya shilingi katika kupunguza rufaa nje ya nchi.
