DMPD (2) KUJENGA BARABARA, STENDI NA MASOKO 18
DAR ES SALAAM:
Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) awamu ya pili utajenga barabara za lami katika Mkoa wa Dar es salaam kilomita 250, kuanzisha mfumo wa udhibiti wa taka ngumu, masoko 18 pamoja na vituo vya mabasi tisa.
Chanzo:- TAMISEMI
Kuelekea utekelezaji wa mradi huo tayari zoezi la kusiani mkataba limefanyika Februari 20 Jijini Dar es salaam, kati ya serikali ya Tanzania kupitia wizara ya fedh na Benki ya Dunia kupitia Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete.
Aidha awamu ya kwanza ya DMDP iliboresha jumla ya kilometa 207 katika halmashauri tatu zilizokuwa chini ya mradi na imeleta mabadiliko makubwa,na Sasa hivi mradi huu utatekelezwa kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Dar es salaam kila halmashauri itajengewa barabara za lami, masoko pamoja na vituo vya mabasi.
Mradi huu unatarajiwa kuboresha miundombinu ya taka ngumu kwa kuanzia katika ukusanyaji, usafirishaji hadi utunzaji wake katika madampo ya kisasa matatu yanatarajiwa kujengwa chini ya mradi huu.
Kadhalika kupitia mradi huo master plan ya mifereji mikubwa ya maji ya mvua itaboreshwa na mifereji muhimu itatambuliwa na itajengewa yenye jumla ya kilometa 90 kwa Dar es Salaam nzima.
#ZINGATIA:-Mradi huo ni ishara kuwa Serikali ina nia thabiti ya kutatua changamoto za miundombinu ya Dar es Salaam na kubadilisha hali ya Jiji la Dar es salaam.