DKT SAMIA NA MBIO ZA KIJITI CHA ELIMU
MARA
Serikali ya awamu ya sita imejipambanua vema mapigano kuhusu elimu pamoja na miundombinu yake, kwa kuendelea kukimbiza mbio hizo Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameidhinisha kiasi cha bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Mara inayojengwa katika eneo la Bulamba, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Shule ya sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Mara inatarajiwa kuchukua wananfunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na hadi sasa ujenzi wa Mabweni na vyumba Vya Madarasa vimekamilika na majengo mengine yanaendelea kujengwa.