DKT SAMIA AZINDUA SANAMU YA BABA WA TAIFA MWL.J.K.NYERERE

 

DKT SAMIA AZINDUA SANAMU YA BABA WA TAIFA MWL.J.K.NYERERE

DKT SAMIA AZINDUA SANAMU YA BABA WA TAIFA MWL.J.K.NYERERE

ETHIOPIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (leo) Februari 18 amezindua Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2024.
Uzinduzi huo umeshuhudiwa na viongozi wengine wa Afrika ambao wamekutana Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhuduhuria mkutano wa 37 wa wakuu wan chi za Afrika ambao pamoja na mambo mengine utaangazia kuhusu amani na usalama wa nchi za Afrika na sera na majawabu kuhusu elimu na ujuzi, ikiwa ni maeneo yanayogusa maisha ya wakazi zaidi ya bilioni moja wa nchi wanachama.
#NguvuyaDiplomasia