RAIS SAMIA KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA
ETHIOPIA
Rais wa JAmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan (leo) tarehe 18 Februari 2024 anatarajiwa kushiriki Mkutano wa 37 wa wakuu wa nchi za Afrika, utakaofanyika katika Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Katika mkutano huo viongozi watajadili kuhusu amani na usalama wa nchi za Afrika, sera na majawabu kuhusu elimu na ujuzi, ikiwa ni maeneo yanayogusa maisha ya wakazi zaidi ya bilioni moja wa nchi wanachama.
Pia mkutano huo unapanga kuzingatia mageuzi ya muundo wa umoja huo,ambapo Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye ameteuliwa kuongoza mchakato wa mageuzi ya kitaasisi ya Umoja wa Afrika (AU), atawasilisha ripoti ya mwisho kuhusu mageuzi ya taasisi hiyo.
Aidha Mambo mengine katika ajenda ni pamoja na suala la ushirikiano wa pande nyingi, lakini pia masuala yanayohusu uchumi na biashara, ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya utekelezaji wa Eneo Huria la Biashara ya Bara la Afrika (ZLECAF).
Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu pamoja na mambo mengine atazindua Sanamu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Makao Makuu ya AU.
