BANDARI YA KABWE YACHOCHEA BIASHARA YA MIPAKANI
RUKWA
Wakulima na wajasiriamali wazawa wa Mkoa wa Rukwa wanavuna matunda ya bandari ya Kabwe kwenye Ziwa Tanganyika ambayo imekuza biashara ya mipakani kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
Bandari hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa pamoja na wakulima wadogo kusambaza bidhaa na huduma katika majimbo ya Moba na Kalemie nchini DRC.
Kuongezeka kwa biashara ya mipakani kumeongeza mzunguko wa fedha na kuinua maisha ya wakazi wa Wilaya ya Nkasi.
Aidha Bandari ya Kabwe inahudumia wastani wa tani 1,200 za mizigo na abiria 400 kwa mwezi, huku asilimia kubwa ikipelekwa DRC.
KUMBUKA:- kabla ya ujenzi wa bandari hiyo wafanyabiashara walikuwa wakipata shida kupata masoko ya uhakika, lakini sasa wanunuzi wanakuja kwenye maeneo yao hivyo kuwahakikishia wakulima masoko ya mazao yao.
