DKT KITIMA (TEC) AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA ZIARA YA VATICAN

 

DKT KITIMA (TEC) AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA ZIARA YA VATICAN

DKT KITIMA (TEC) AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA ZIARA YA VATICAN

DAR ES SALAAM
Ikiwa ni siku chache zimepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan afanye ziara mjini Vatican kwa mwaliko wa Baba mtakatifu Papa Francis Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Dkt Charlse Kitima amesema ziara hiyo iliashiria dhamira ya Tanzania katika kukuza uhuru wa kidini ambao umekuwa ukiimarisha amani na mshikamano wa kijamii kwa ajili ya ustawi wa watu wote.
Pia Dkt Kitima amesema kuwa uhuru wa dini umewezesha dini mbalimbali likiwemo Kanisa Katoliki kufanya shughuli zao za kiroho vizuri sambamba na kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Amebainisha kuwa miundombinu ya kijamii inayohitajika, ikiwa ni pamoja na shule na hospitali, inatoa huduma bora bila ubaguzi.
“uhuru huo umeiweka Tanzania katika orodha ya kimataifa ya Papa ya nchi zinazohakikisha uvumilivu wa kidini na kushirikiana na taasisi za kidini kuboresha maisha ya wananchi,"Ninaipongeza serikali yetu kwa kutekeleza sera endelevu ya mtangamano ambayo inaunganisha dini zote," Amesema Dkt Kitima.
Ameongeza “ziara hiyo inaitambulisha Tanzania kuwa ni balozi mwema wa amani wa kikanda na bara, jambo ambalo nchi nyingine zinaweza kuiga”
#Uongoziunaoachaalama